Tone la Damu na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi kumi (10) bora za mzunguko wa tano (5) 2018 wa Andika na Soma, shindano la hadithi fupi kwa wanafunzi wa shule za sekondari Tanzania. Shindano hili lilibuniwa na kuendeshwa na Taasisi ya Usomaji na Maendeleo –Soma ili kuibua na kuchipuza vipaji vya uandishi wa kubuni miongoni mwa vijana; kuamsha ari ya usomaji na uandishi; na kuwawezesha vijana kutumia uandishi wa kubuni kujadili masuala yanayowahusu wao, jamii zao, taifa na ulimwengu.
- Hadithi Zilizomo:
- Tabu Tabuni
- Msitu wa Ajabu
- Safari ya Matumaini
- Tone la Damu
- Lazima Nifanikiwe
- Shamba la Dhahabu
- Misukosuko
- Hatima ya Mtemi
- Mifupa Hai
- Mtaa wa Hekaheka
Waandishi wa toleo hili ni: Otilia Haule kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Luise na mshindi wa kwanza (Tabu Tabuni); Irene Magayane kutoka Shule ya Sekondari Dar es salaam, mshindi wa pili (KE) (Msitu wa Ajabu); Ayubu Mashaka kutoka shule ya sekondari Benjamini William Mkapa, mshindi wa pili (ME) (Safari ya Matumaini); Emmauel Minja kutoka Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa , mshindi wa tatu (ME) (Tone la Damu); na Cecilia Mgimbira, kutoka Shule ya Sekondari Madibira, mshindi wa tatu (KE) (Lazima Nifanikiwe). Wengine ni: Aidani Mtura kutoka Shule ya Wavulana Tabora (Shamba la Dhahabu); Thandi Mtema kutoka Shule ya Sekondari Irkisongo (Misukosuko); Mashaka Said Malilo, kutoka Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora (Hatima ya Mtemi); Alfeji Daimoni kutoka Shule ya Sekondari Madibira (Mifupa Hai); na Robert Mwijonge kutoka Shule ya Sekondari Madibira (Mtaa wa Heka Heka).