Maida Wairi Juma ni mwanamke Jasiri ambaye amethubutu kupasua mfumo dume nchini Tanzania kwa kujikita katika shughuli za ukandarasi na kujizolea tuzo kutokana na umahiri wake katika ukandarasi na ujasiriamali.
Akiongoza kwa ustadi mkubwa kampuni yake ya Ibra Contractors Limited, ambayo hujenga majengo, barabara na miundombinu mbalimbali ikiwemo madaraja amekuwa na mafanikio makubwa kuigwa mfano na wanawake wengine wanaojiingiza katika shughuli za ukandarasi.