Riwaya ya Mungu Hakopeshwi ni riwaya iliyoshinda na kupewa tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2018.
Riwaya hii inaelezea maisha ya familia moja ya Unguja iliyoingia katika mitafaruku na mikasa mingi.
Kila kitu huwa na chanzo na khatima; basi ni nini chanzo cha mitafaruku hiyo na khatima yake ilikuwaje?
Simulizi ni juu ya baba, Bw. Ahmed, mwenye hasira kali zisizo na mipaka, aliyeongoza familia yake kwa utashi wa nafsi yake, bila kujali hisia za mkewe wala wanawe. Kumbe moyoni mwake alihifadhi siri, na hiyo siri ndiyo iliyomfanya Bw. Ahmed kuwa mkali bila kiasi, ikimsukuma azuie kurejea kwa yale yaliyomfika zamani. Lakini kivuli cha historia ya maisha yake ya nyuma hakikuacha kumuandama.
Riwaya hii imeandikwa kwa lugha nzuri na fasaha, kwa ufundi wa msanii makini na mwelewa wa maisha ya jamii za Kizanzibari na za mwambao kwa jumla