Mtoto wa Mama ni riwaya inayotoa taswira ya maisha ya familia ya mzazi mmoja, Zamda na mtoto wake, saburi. wote wamepotelewa, Zamda na mume wake Shauri, na Shauri na baba yake. Hawajui kama yu hai au kafa.
Walipojua, tayari Jalala,mtawala mkuu wa nchi alikuwa tayari amemhukumu Shauuri adhabu ya kifo kwa kunyongwa hadharani. Kabla ya hukumu hiyo kutekelezwa, Shauri tayari kitanzi kimemzunguka rohoni.