Tamthilia hii, ambayo inatokana na riwaya, The Money Order, iliyoandikwa na mwandishi mashuhuri wa Senegal, Sembene Ousmane, inajadili mfumo wa umangi–meza uliorithiwa na nchi nyingi za Afrika kutoka kwa Wakoloni pamoja na athari zake kwa jamii. Ibrahim Chande anafurahi sana anapopokea hawala ya shilingi 2,000/= kutoka kwa mpwaye aliyeko masomoni Landani. Lakini anashindwa kuzuia habari hizo nzuri kuwafikia majirani na watu wenye maduka mtaani kwao. Wote wanamzengea wakitazamia chochote kutokana na fedha hizo, licha ya kwamba zote si zake. Hata hivyo, matatizo ya urasimu yanajiingiza kati yake na fedha hizo.
Format | Paperback |
---|---|
Language | Swahili |
Publisher | Mkuki na Nyota |
ISBN | 9789987753918 |
Author | Amandina Lihamba |