Punda waliishi huru kabisa katika nchi yao wenyewe iliyoneemeka kwa kila hali. Waliishi na Malkia wao aliyeitwa Fari. Mvua zilinyesha vizuri. Punda walikula na kusaza. Mito, maziwa na mabwawa, yalijaa maji tele. Lakini haukupita muda punda mambo yaliwageuka. Je, kitu gani kilitokea kilichowanyang’anya punda uhuru wao huo na neema zao hizo na kuwafanya watumwa wa kazi zetu sisi binadamu leo hii? Je, yapo mafunzo tunayoweza kupata kutokana na yaliyowasibu punda? Utapata majibu ya maswali haya katika hadithi hii iliyo na mengi yaliyotokea, iliyoandikwa na Tololwa M Mollel, mwandishi wa vitabu vingi vya watoto.
Hadithi ya Punda na Malkia wao Fari
Sh7,500
Format | Paperback |
---|---|
Language | Swahili |
Publisher | Mkuki na Nyota |
Author | Tololwa M Mollel |