Juma Hamisi, Muislam safi kutoka Bagamoyo anafariki na roho yake inaenda Mbinguni. Baadaye inafahamika kuwa hili ni kosa kubwa lililofanywa na Ziraili, Malaika mtoa roho. John Houghton wa Uingereza ndiye aliyestahili kutolewa roho siku hiyo. Ili kutatua tatizo hili, roho ya Juma Hamisi inabidi irudishwe duniani. Baada ya majadiliano ya muda na ili kuficha kosa hili lisigunduliwe, Ziraili na wenzake wanakubaliana kuirudisha roho ya Juma katika mwili mwingine, hata kama ni mwili wa paka
Format | Paperback |
---|---|
Language | Swahili |
Publisher | Mkuki na Nyota |
Author | Farouk Topan |