Usomaji kwa watoto ni shughuli mojawapo katika mikakati ya taasisi yetu Kuelekea kuwa na maktaba ya jamii. Hivyo basi mwaka jana tuliadhimia tuanzie nyumbani ambapo tulikuwa na kijiwe cha usomaji eneo la Mikocheni A. Mtaa wa Michungwani , tulikuwa tunakusanyika pamoja na watoto walioko mashuleni na majumbani kila Jumatano na Jumamosi kwa ajili ya kujisomea kwa maana ya maktaba ya watoto.
- Tulitembelea majumbani kuwaelezea wazazi na watoto uwepo na umuhimu wa hiki kijiwe cha usomaji,
Tulisoma vitabu, Tulifanikiwa kusoma vitabu vingi kama vile;
1. Mlima wenye dhahabu
2. Kunguru mvuvi hodari
3. Ndoto ya Lulu
4. Mama mbeku
5. Nyamanza Ndege wa Amani
6. Nyani Mtu
7.Simu ya Mwanambweha
8. Jogoo na Kanga
9. Mtoto Aliyetelekezwa
10. Nora na Matunda ya Ajabu
11. Majivuno Yamuua Samaki
12. Sisimizi Amuua Tembo
- Maigizo kutokana na dhima na ujumbe, ktk usomaji wa vitabu,
- Tulijadili kitabu,
Tuliibua mijadala baada ya kusoma kitabu , kuvaa uhusika wa mwamdishi wa kitabu , na wahusika wa kwenye kitabu, kuoainisha hali halisi ya jamii.
- Michezo mbalimbali , ya shule na ya kubuni,
Tulicheza mpira wa miguu, mpira wa mikono ,michezo ya kubuni mingine ni kwa ajili ya kuweka uelewa na kumbukumbuku kwa vile tunavyovifanya
- Tulichora kuhusiana na kitabu,
Tulichora picha na maumbo mbali mbali kutokana na picha za kwenye vitabu tulivyosoma, na picha za kubuni kutokana na hadithi, mfano kitabu cha” Mama Mbeku” watoto walijaribu kuchanganya rangi, ” Nora na Matunda ya Ajabu” walichora matunda mbalimbali,
- Tulibuni hadithi nyingine kuhusiana na hadithi husika,
Watoto walibuni hadithi zao wenyewe, hadithi kutokana na kichwa cha habari cha hadithi , hadithi kutokana na ujumbe , muendelezo wa hadithi kwa kupokezana.
- Mpira ni wa nani,
Ni shughuli ambayo lengo kuu ni kuleta ushirikiano,umiliki wa kijiwe ambapo ilianza kwa kutengeneza mpira kwa pamoja na kuutumia kwa kucheza na kuutunza
- Nyumbani kwetu,
Tulianzisha shughuli hii kwa lengo la kujua mazingira ya nyumbani,- background za watoto
Tulichora picha za mazingira ya nyumbani kwa kuelezea kila picha
tulipeana kazi za nyumbani zilizochochea mtoto kumhoji mzazi kudadisi na kujua zaidi kuhusu jamii yao
- Kujiwezesha/uwezeshwaji,
Tullisaidia katika kujiwezesha – kuchagua kitabu cha kusoma kwa pamoja watoto walichagua wawezeshaji ambao walikuwa viongozi kwa kila kipindi wawezeshaji waliochaguliwa walisimamia na kusoma kuuliza maswali, k itabu kieleweke kwa kila mmoja
- Ufahamu utungaji, ufupisho,maswali na majibu
Baada ya kusoma vitabu tulitunga hadithi kutokana na uelewa wa hadithi tulizosoma, tulifupisha /muhutasari wa hadithi, tulisomeana imla ktk kipengele kimojawapo cha hadithi, tuliulizana maswali ya ufahamu baada ya kusoma hadithi katika kukazia uelewa.
Kijiwe cha usomaji kwa watoto 2014
Kwa mwaka huu tumepanga zoezi hili lishirikishe watoto kutoka sehemu mbalimbali, hivyo basi kama wewe ni baba, mama, dada, kaka tunakuomba uwahimize watoto na wadogo kuja kusoma na wenzao!
Muda: Jumamosi saa 9 alasiri mpaka saa 11 jioni.